Mzee wa tafakari

Tuesday, February 06, 2007

Bajeti ya mwaka huu iboreshe maisha ya watanzania

WAZIRI wa Fedha, Zakia Meghji wiki hii alitoa sura ya bajeti ya serikali ya mwaka ujao ikionyesha kuwa jumla ya Sh4.8 trilioni zitatumika katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Waziri alieleza kuwa bajeti ya mwaka ujoa imejengwa katika misingi ya ilani ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na kwamba fedha zitapelekwa katika maeneo ambayo muhimu kwa ajili ya kuboresha maisha ya watanzania.

Kati ya fedha hizo, kiasi kikubwa kikiwa kimeelekezwa kwa Wizara za Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kilimo, Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Usalama wa Raia, Afya na Ustawi wa Jamii na Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Katika bajeti hiyo, Sh3.1 trioni zimetengwa kwa matumizi ya kawada wakati 1.7 trilioni miradi ya maendeleo. Katika bajeti hiyo ambayo itatangazwa Juni 15, Sekta ya Kilimo imepewa kipaumbele zaidi kwa kupatiwa jumla ya sh bilioni 333.

Katika bajeti ya mwaka 2005/2006 serikali ilitenga kutuymia sh trioni 4.17. Kwa maana hiyo kuna ongezeko kidogo katika bajeti ya mwaka huu.

Sio nia yangu kuanza kuchambua takwimu zote zilizopo katika sura hiyo ya bajeti bali ninataka kuwapa wasomaji wangu angalu kwa muhtasari bajeti hii ilivyo.

Baadhi ya shughuli muhimu ambazo zimepatiwa mgawo zaidi wa fedha kwa kuzingatia ilani ya uchaguzi wa CCM ni hifadhi ya mazingira iliyopata sh bilioni 9.4, ruzuku 21 badala ya sh bilioni saba mwaka jana.

Pia bajeti ya mwaka ujao kwa mujibu wa Meghji serikali imetenga kwa ajili ya kuwapandishia mishahara watumishi wake.

Ingawa serikali inalenga kukusanya mapato ya ndani yasiyopungua Sh trilioni2.5 trilioni ikilinganishwa na mapato ya Sh2.06 ya mwaka 2005/06. Ongezeko hilo litakuwa ni asilimia 19.1.

Kwa hakika kuongezwa kwa bajeti ya kilimo kutasaidia kuwapatia ajira watu wengi zaidi vijijini.

Hata hivyo, ingawa serikali imeongeza fungu katika kilimo kama hakutakuwa na mikakati mizuri ya namna ya kuwapunguzia umasikini wananchi kwa kutumia rasmali zetu hazitasaidia kitu.

Kwa mfano hivi sasa mabebki mengi nchini hayawezi kutoa mikopo kwa wakulima wadogo kutokana na kuwa na sera ambazo zinahitaji mtu kuwa na dhamana kubwa.

Je mkulima wa jembe la mkono aliyeko mbinga ataweza kukwamua vipi na umasikini kama hataweza kuwa na uwezo wa kwenda kukopa benki kupata mtaji utakaomwezesha kupanua kilimo chake?

Kwa upande wa hela azilizotengwa kwa ajili ya ruzuku ya mbolea, bado nako kwa upande hakuna usimamizi mzuri wa usamabaji wa mbolea hii.

Tunaendelea kushuhudia mbolea ya ruzuku kwa wakulima wa mikoa ya nyanda za juu kusini wanalia kuwa wanauziuwa mbolea hiyo na wafanyabiashara kwa bei ya juu ambayo hiana punguzo.

Kwa upande wa ogezeko la la mapato ya ndani, ingawa serikali imesema kuwa katika bajeti ijayo inatarajia kuongeza mapato ya ndani ya kwa asilimia 19.1 kutoka sh trioni 2.06 hadi sh trioni 2.4, misamaha ya kodi inayotolewa na serikali kwa waagizaji wa bidhaa kutoka nje inapunguza mapato haya.

Hivi sasa taarifa zilizopo zionanyesha kuwa karibu asilimia 30 hadi 40 ya makusanyo ya ndani kwa mwezi hurudishwa kwa walipokodi kama misamaha ya kodi.

Nadhani kuna umuhimu sasa sheria ya misamaha ya kodi ikarekebishwa ili baadhi ya watu au taasisi zikaondolewa katika misamaha ya kodi.

Hivi sasa watu wengi wanatumia mwanya huo, wa kuwapo kwa mlolongo wa makundi mengi yanayoruhusiwa kupewa misamaha ya ushuru wa forodha kukwepa kulipa ushuru na hivyo kuikosesha mapato serikali.

Suala jingine ambalo nadhani ni muhiumu katika bajeti hii likaangaliwa kwa umakini ni ubadhilifu wa fedha za mabilioni katika halmashasuri.

Ingawa serikali imeeleza katika bajeti ya mwaka ujao itaajiri wahasibu wawili kwa kila halmashauri ili kuongeza udhibiti wa fedha kupotea, lakini watumishi hao nao hawaagaliwa kwa karibu nao watataweza kuzitafutana fedha hizi za walipa kodi.

Tatizop la ulaji wa fedha katika halmashauri ni kubwa na kwamba baadhi ya mawadiwani kwa kushirikiana na wakurugenzi wa halamshauri hushirikiana kuweka matumizi hewa na fedha hizo kuingia mifukoni mwao.

Ni vyema sasa serikali ikawaeka utaratibu unaowabana watendaji wa halamshauri kutafuna fedha.

Suala jingine ambalo katika bajeti hii tunaomba lifanyiwe kazi ni
Kwa vitambulisho vya urai. Sisi wananchi tunashindwa kuelewa nini kinachokwamnisha suala hili licha ya serikali kueleza kila mara kuwa inaendelea na mchakato wa utekelezaji.

0 Comments:

Post a Comment

<< Home