Karume kubali serikali ya mseto yaishe!
UCHAGUZI wa rais, wabunge na masheha visiwani Zanzibar uliofanyika Jumapili iliyopita ulifikia ukingoni Jumanne wiki hii baada ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kumtangaza Rais Aman Karume kuwa ndiye mshindi wa kiti cha urais.
Kwa mujibu wa ZEC, Karume alishinda kwa asilimia 53.2 akiwa mbele ya mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Sharrif Hamad aliyepata asilimia 46.1 ya kura zote zilizopigwa.
Karume aliapishwa asubuhi ya siku hiyo katika sherehe zilizohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ya Muungano na baadhi za mabalozi zilizopo hapa nchini.
Hata hivyo, uchaguzi huo, ulitawaliwa na dosari kadhaa zikiwamo za baadhi ya wapigakura kushindwa kuona majina yao vituoni, baadhi ya vituo kuchelewa kufunguliwa na baadhi ya watu kugundulika kuwa walitaka kupiga kura mara mbili.
Tayari Marekani imesema haijafikia uamuzi wa kukubali kuwa uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa huru na haki, mpaka tuhuma zilizojitokeza za ukiukwaji mkubwa wa taratibu za kupiga kura zitakapofafanuliwa.
Taarifa ya ubalozi wa Marekani kwa vyombo vya habari, nchi hiyo imesema haikuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Karume kwa sababu kuna mambo ambayo hajawekwa wazi kuhusu uchaguzi huo.
Ubalozi huo umesema kwamba ingawa wanapongeza uboreshaji ulioonekana katika mchakato mzima wa uchaguzi wa Zanzibar, ukilinganishwa na ule uliokuwapo wakati wa uchaguzi wa 2000.
Bado wanatiwa mashaka na ukiukwaji mkubwa ulioshuhudiwa na waangalizi wa kimataifa, ikiwamo taasisi ya National Democratic Institute (NDI).
Kutokana na hali hiyo, Marekani imejitoa katika kundi la nchi na taasisi zilizotoa tamko kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.
Hata hivyo, kwa upande wake Serikali ya mapinduzi Zanzibar imepinga vikali taarifa hiyo kwa maelezo kuwa kama waangalizi wote wa nje wamesema ulikuwa huru na haki iweje kwa iwe kwa Marekani tu. Wameitaka serikali ya Marekani kuacha kungilia masulaa ya ndani ya Zanzibar.
Sio nia yangu leo katika safu hii kuangalia dosari zilizojitokeza ila ninachotaka kuzungumzia ni suala la serikali ya umoja.
Baada ya Rais Karume kuapishwa alifanya mkutano na waandishi wa habari na kueleza wazi msimamo wake kuwa hayupo tayari hivi sasa kuunda serikali ya mseto ambayo inawashirikisha CUF.
Karume bila ya kusita alisema katika utawala wake hana wazo la kuunda serikali ya mseto kwa kushirikisha watu kutoka vyama vya upinzani.
Kwa hakika kauli hiyo ya Karume inazusha maswali mengi ya kujiuliza iwapo kiongozi huyo ameyasema hayo dhati kutoka katika sakafu ya moyo wake au la!.
Inaniwia vigumu kuamini kuwa Karume alisema hayo kwa dhati kutokana na hali tete ya Zanzibar ilivyo hivi sasa.
Suala la serikali ya mseto haliwezi kukwepeka kutokana na wapinzani kupata kura nyingi. Kuwaacha nje ya karibu nusu ya wazanzibari katika utawala ni kuendelea kuzusha migogoro isiyofaa.
Najua kuwa Maalim Seif tayari amekataa kuyatambua matokeo ya uchaguzi kwa madai kuwa chama chake ndicho kilichoshinda katika uchaguzi huo, lakini hiyo haikuwa sababu ya Karume kuwa na msimamo ambao unaonyesha kuendeleza ufa miongoni mwa wazazibari.
Kudharau wapinzania ambao wamepata asilimia 46.1 ya kura zote zilizopigwa ni kuwadharu karibu nusu ya wazanazibari ambao waliwapigia kura wapinzania.
Ubinafsisi wa kung'angnia madaraka katika enzi hizi iumepitwa na wakati. kinachotakiwa kufanyika hivi sasa kwa Karume ni kukubali kuunda serikali ya mseto ili kumaliza matatizo ya mgawanyiko yaliyopo hivi sasa visiwani humo.
Ushauri wa serikali ya mapinduzi Zanzibar kuunda serikali itakayowashirikisha wapinzani umeanza kutolewa siku nyingi na watu mbalimbali wakiwamo Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Mwalimu Nyerere baada ya uchaguzi wa 1995 alimshauri Rais Salmin Amour aunde serikali ya mseto lakini hakusikiliza ushauri huo, hali ambayo iliendeleza migogoro mingi ya kisiasa.
Vile vile, wapo watu mbalimbali ambao wamekuwa wakishauri kuwepo kwa serikali ya mseto lakini inaonekana suala hilo kwa watalawa wanaoigia madarakani hawataki kulisikia hali ambayo ndio imekuwa chanzo cha matatizo mengi yalizoaa mwafaka wa CCM na CUF.
Kutokana na Karume kutangaza rasimi msimamo wake mapema, kinachoonekana ni kuwa visiwa hivyo vitaendelea kuwa na vurugu huenda mwafaka wa tatu kati ya CCM na CUF ukasainiwa tena.
Karume mtaingia mwafaka mara ngapi? kubali yaishe.
0 Comments:
Post a Comment
<< Home