Wanaohujumu miundombinu ya maji ni watanzania?
WIKI iliyopita Mahakama ya mwanzo ya Manzese iliwahukumu wakazi wawili wa jijini Dar es Salaam kwenda jela miaka mitano kila mmoja kwa wizi wa mali ya Shirika la Uendeshaji la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) yenye thamani ya sh milioni 1.5.
Watu hao wamefungwa baada ya kupatikana na kosa la wizi wa vifaa vya air valve, washout tatu na mita ya maji.
Katika hukumu yake hakimu mfawidhi Mariam Masamalu alisema anatoa adhabu hiyo kali kwa washitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine ambao wamekuwa na tabia ya kuhujumua miundo mbiunu ya maji nchini na kwamba mara baada ya kumaliza kifungo gerezani itabidi warejeshe thamani ya mali ya DAWASCO.
Kwa hakika, hukumu hiyo imesaidia kuwakumbusha watanzania wenye mazoea ya kuhujumu miumdo mbinu ya maira ya maendeleo kuwa serikali ina mikono mirefu na kwamba haijalala.
Vitendo vya kuhujumu miundombinu ya miradi ya maendeleo ikiwamo ya DAWASCO imekuwa kawaida kwa baadhi ya watanzania.
Baadhi ya watu wanadiriki hata kukata nyaya za umeme zenye moto na wengine wanajiunganishia maji kwenye bomba kuu na kuiba mita za maji bila ya kujali kwa kufanya hivyo ni kuzipunguzia mamlaka zinazohusika uwezo wa kutoa huduma kwa wananchi.
Sio siku nyingi vyombo vya habari viliripoti kuwa kuna mkazi mmoja Buruguni jijini Dar es Salaam alikuwa ameuganisha bomba lake la majitaka katika bomba la majisafi la DAWASCO. Habari hiyo ilishitua watu wengi sana kusikia kuwa kuna mwenzetu ambaye alikuwa ameamua sio kuhujumu tu mamlaka ya maji bali hata kuua wakazi wenzake kwa kuwanyesha kinyesi cha familia yake.
Haingii haraka akilini kuelewa mtu huyo alikuwa na lengo lipi kuchukua uamuzi huo. Nadhani vitendo kama hivi vinapaswa kudhibitiwa na kulaaniwa kwa vile ni kitendo ambacho sio tu harasa kwa DAWACO bali kinaweza kusaabisha kifo kwa mamia ya watu wanaoishi katika eneo hilo.
Tukio hilo limetuonyesha kuwa huenda sababu kubwa ya kipindupindu kuweka makazi yake maeneo ya buruguruni, vingunguti na ilala na Mwanyamala huenda wapo watu wengi wanaofanya hujuma kaa hizo katika miundombinu ya mamlaka ya maji.
DAWASCO kwa muda mrefu imekuwa ikilalamikia vitendo vya baadhi ya watu kuhujumu miundombinu yake kwa kuiba vifaa ya kuwezesha usambazaji wa maji na wengine kujiunganishia maji kienyeji ambayo wamekuwa wakiyatumia bila ya kulipia huduma hiyo.
Ni jambo la kushangaza kuwa sisi wananchi tunashiriki katika hujuma hizi za kujiuganishia maji kinyemela na kuiba vipuri vya kusaidia usambazaji wa maji, lakini ndio tumekuwa mbele kulalamika kuwa hatupati maji ya uhakika.
Tuelewe kuwa mamlaka za maji nchini zinajiendesha kwa kutumia mapato yanaypotokana na makusanyo ya ankara za huduma za maji, kama watanzania wengi tutatumia ujanja unjanja wa kupata maji bila ya kulipia na kuiba vipuri vya miundo mbinu, taasisi hizo zitajiendesha vipi?
Ni wazi kuwa utamanduni wa kuiba na kuharibu miundombinu ya miradi mbalimbali haitatufikisha mahali kokote watanzania . Sasa umefika wakati kwa kushirikiana na mamlaka hizo, vyombo vya dola watanzania wote kila mmoja awe mlinzi wa mali za umma ili akimwona mtu anayehujuma atoe taarifa polisi au ofisi za serikali.
Bila ya kuwa na uzalendo wa aina hiyo, miundomibinu yetu itaendelea kuhujumiwa na watu wachache kwa manufaa yao binafsi huku wakituacha tukiwa hatupati huduma.
Tukiacha hivi hivi, sio ajabu siku moja hata mtambo wa kusukuma maji wa Ruvu chini mkoani Pwani nao ukahujumiwa.
Hukumu iliyotolewa kwa wakazi wawili wa jijini kwenda jela kifungo cha miaka mitano kutokana na kuhujumu miumndombinu ya DAWASCO nadhani itatoa fundisho kuwa sasa ukichezea mali ya miradi ya maendeleo utakiona cha moto.
Haiwezekani katika nchi ambayo inafuata utawala wa sheria mtu ajiamulie kufanya analotaka hata kama litakuwa la kurudisha maendeleo nyuma, kuiba mita mabomba ya maji au nyaya za umeme ni uhuni ambao unapaswa kukemewa na wapenda maendeleo wote.
Watanzania ni watu ambao wanapenda sana maendeleo, lakini baadhi ya wanzetu bado na wakasumba za enzi ya ujamaa kuamini kuwa mali ya shirika la umma haina mwenyewe unaweza kujichukjulia tu.
Kasumba hii ndio ambayo kwa kiasi kikubwa ilifanya baadhi ya mashirika na makampuni ya umma ya umma tuliyokuwa tukiyaendesha kufa na mengine kujiendesha kwa hasara kutokana na watendaji wake na wananchi kujichukulia mali zake wakidai ni za umma.
0 Comments:
Post a Comment
<< Home