Mzee wa tafakari

Tuesday, February 06, 2007

Mwacheni Hamad apige kura


WIKI hii joto la Uchaguzi Mkuu wa rais na wabunge unaotarajiwa kufanyika Oktoba 30 mwaka huu nchini
lilimwuguza Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Shariff Hamad ambaye katika hali isiyokuwa ya
kawaida alizuiwa kujiandikisha katika Daftari la Wapigakura visiwani Zanzibar kwa madai kuwa sio mkazi
wa eneo hilo.

Tukio hilo lilitokea katika Kituo cha uandikishaji cha Mtoni Kidatu kilichopo jirani na nyumbani kwa
Hamad baada ya Msimamizi wa kituo hicho Suleiman Ame kueleza kuwa kiongozi huyo wa Chama cha upinzani
hawezi kumwandikisha kwa sababu hana sifa ya ukaazi wa kawaida katika eneo hilo.

Msimamizi huyo alisema kuwa ili mtu aweze kuwa na sifa ya kuandikishwa katika daftari la wapiga kura ,
anatakiwa awe ameishi katika jimbo husika kwa muda wa miezi 36 mfululizo na kwamba kipengele hicho ndicho
kinachombana Hamad kuandikishwa.

Naye Sheha wa Shehia ya Mtoni Kidatu, Haji Abdulrahma alisema pamoja na kuwa anamtambua Hamad,
lakisi si mkazi wa eneo hilo kwa vile hajakaa hapo kwa
miezi 36 mfululizo.

Alisema mara nyingi amekuwa akimpelekea Maalm Seif barua mbalimbali za wito na nyingine za kumtaka
ashiriki katika shughuli za maendeleo za Shehia yake,lakini amekuwa haonekani na kwamba amekuwa haishi
katika nyumba yake.

Sheha huyo alikwenda mbali zaidi na kudia kuwa katika kuonyesha kuwa Hamad haishi katika eneo hilo hata
matangazo ya vifo ambayo amekuwa akitumiwa salama yamekuwa yakieleza kuwa habari hizi zimfikie mahali
kokote alipo.

Tukio hilo la kuzuiwa kujiandikisha kwa Maalim Seif ambaye pia ni Waziri Kiongozi Mstaafu linashangaza,
kwa sababu hakuna mtu asiyejua kuwa Hamad ni mkazi eneo hilo kwa nini leo anaonekana kuwa sio mkazi?

Mzengwe huo uliofanywa na msimamizi wa kituo cha uandikishaji wapigakura kumzuia Hamad kuajinadikisha
ni dhahiri ni chokochoko zinazofanywa kwa ajili ya kuzusha vurugu nyingine visiwani.

Ni juzi tu watu wartatu walijeruhiwa huku mmoja wao Khamis Juma Issa akielezwa kuwa katika hali mbaya
baada ya kuzuka vurugu katika kituo cha unadikishaji wapiga kura cha Kikuni Chemchem katika jimbo la Mwera,
Mkoa wa Mjini Magharibi.

Nasema ni tukio lilifanywa makusudi kwa ajili ya kuchochea ghasia kwa sababu maelezo yaliyotolewa na
Msimamizi kumzuia Hamad kuandikishwa hayana uzito wowote zaidi ya kujaa siasa zenye chuki.

Huwezi kusema kuwa Hamad sio mkazi wa eneo hilo eti kwa sababu amekuwa hashiriki katika shughuli za
maendeleo za eneo analokaa na kwamba amekuwa haonekani
mtaani.

Msimamizi wa Kituo cha Uandikishaji anapaswa kuelewa kuwa Hamad ingawa hayupo tena kwenye utumishi wa
serikali ni Katibu Mkuu wa chama cha siasa ambaye ana majukumu mbalimbali yanayomfanya asafiri mara kwa mara
badala ya kukaa barazani akicheza bao.

Hakuna kiongozi wa chama kikubwa cha siasa ambaye anaelewa majukumu yake anaweza kushinda barazini
akinywa kahawa na kula tende na harua kila siku labda atakuwa anaendesha familia na sio chama.

Hata ukiwa kiongozi wa familia huwezi kushinda kutwa nzima kila siku barazini ukipiga gumzo bila ya kutoka
kwenda kutafuta chochote, vinginevyo utakuwa unafanya biashara ya ajabu isiyoeleweka.

Hivyo, Suleiman na wenzake wanapaswa kuelewa kwa wadhifa wake Hamad lazima asafiri kwenda jijini Dar es
salaam na hata nje ya nchi kwa ajili ya kuhudhuria washa , mikutano ya kimataifa na shughuli nyungine.

Nafikiri Mheshimiwa Suleiman anataka kuifananisha kazi ya Usimamizi wa uchaguzi au usheha, na ukatibu Mkuu wa
chama, kitu ambacho hakifanani kabisa! Hata makatibu wengi wa vyama vya siasa hapa nchini kama vile Philip
Mangula (CCM), Polisya Mwaiseja (NCCR-Mageuzi), Dk. Wilbroad Slaa (CHADEMA) hawaonekana kila siku barazani
kwenye nyumba zao, wanashughuli nyingi mno zinazowafanya hata wasahau kula chakula.

Vile vile, kwa upande wa madai kuwa Hamad sio mkazi wa eneo hilo kwa sababu hata anapotumiwa salama za
vifo wanaomtumia wamekuwa wakieleza kuwa habari zimfikie mahali popote alipo, ni sababu za kitoto
ambazo zinaonyesha sasa siasa za Zanzibar zinakwenda upogo.

Kwani mtu kumtumia taarifa za msiba na kueleza kuwa habari zimfike mahali alipo ni kuwa hajulikani
anapoishi? Nadhani sasa umefika wakati ambao Wazanzibar mpaswa kukaa na kuelewa kuwa vurugu
zinazotokea zinasababishwa na nyinyi wenyewe.

Maalim Seif hata kama ana makosa yake basi anapswa kuadhibiwa kwa yale aliyotenda sio haya ya kuwekewa
mizengwe ya kujiandikisha wakati ukweli upo wazi kuwa
ni mkazi wa eneo hilo.

Kwa upande wake Hamad anapaswa naye kudhibiti baadhi ya wafuasi wake ambao wamekuwa wakidaiwa kufanya
chokochoko kadhaa katika maeneo ya kujiandikishia wapigakura ili kuepusha Zanzibar katika umwagaji wa
damu.

Wakati dunia imekodolea macho Uchaguzi wa rais na wabunge Zanzibar kutokana na historia ya nyuma , CUF
na CCM wanapswa sasa kuwatuliza wanachama wao kupunguza munkari ili uchaguzi ufanyike kwa njia ya
utulivu zaidi.

Hivi sasa dalili za kuzuka vurugu zimeanza kuonekana kutokana na matukio ya vurugu na watu kujeruhiwa
wakati huu wa kujiandikisha kupiga kura. Kama sasa watu wameanza kujeruhiana itakuwaje wakati wa uchaguzi
wenyewe nafikiri itakuwa kuchinjana. Hilo hatulitaki liotokee kabisaa!

0 Comments:

Post a Comment

<< Home