Mzee wa tafakari

Tuesday, February 06, 2007

Mipango hii ifanikiwa basi isiwe longolongo

WIKI hii serikali ilitamka bungeni kuwa inafanya jitihada za kushirikiana na kampuni moja ya China kuzalisha gesi iliyosindikwa ili iweze kutumika kama mafuta ya magari badala ya petroli na dizeli.

Uamuzi huo wa serikali unatokana na baadhi ya wawekezaji waliopatikana mwaka 2004 na mwaka jana wa kuzalisha gesi iliyosindikwa kuiwekea masharti mbalimbali serikali.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Lawrence Masha aliliambia bunge kuwa China imepiga hatua kubwa katika teknolojia hiyo na tayari ujumbe wa Shirika la Maendeleo la Petroli (TPDC) limeitembelea nchi hiyo Novemba mwaka jana.

Alisema nchi hiyo pia imekubali tena kugharimia ujumbe mwingine wa Mei mwaka huu wa kujifunza kuhusu teknolojia na sera za China zilizowezesha mafanikio makubwa katika utumiaji wa gesi asilia, sio tu kwenye magari lakini pia utumiaji wa gesi asilia kwa ajili ya kupikia majumbani na kwenye taasisi.

Kampuni ya awali iliyopatikana mwaka 2004 mwekezaji huyo aliweka sharti kwamba kampuni nyingine zisihusike katika usambazaji wa gesi hiyo badala yake yeye ndiye pekee aruhusiwe kufanya hivyo.

Kwa hakika habari hiyo ni njema, kwa sababu itatuwezesha watanzania kupata mafuta ya kuendeshea magari na mitambo kwa urahisi na kwa bei nafuu.

Nasema habari hii ni njema kwa sababu hakuna sababu yoyote ya sisi watanzania kupata tabu ya kununua mafuta kutoka urabuni wakati tuna nishati mbadala ya gesi ambayo inaweza kutumika kama mafuta.

Nadhani hata wazoi hili la kuanza kuitumia gesi tunayozalishaji kutoka Songosongo na Mnazi bay baadaye kwa ajili ya kuendeshea magari limechelewa kutolewa kutokana na ukweli kwamba nishati hii mbadala, tunaihitaji kwa udi na uvumba suku nyingi.

Kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia ni moja ya sababu kubwa ya kupanda kwa gharama za uzalishaji wa bidhaa nchini. watanzania hatuna haja ya kuathirika na bei ya mafuta katika soko la dunia wakati mwenyezi Mungu ametujalia kuwa na gesi asili ambayo tunaweza kuitumia kama mafuta.

Ni jambo la ajabu sana watanzania kulia kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia wakati, sisi tuna hazina kubwa ya nishati ambayo tayari tumeanza kuitumia.

Hii ni sawa na hadithi ya mabahari waliokuwa wakisafiri na meli katika mto mkubwa sana walioishiwa na maji ya kunywa wakaomba msaada wa kuletwa maji wakifikiria kuwa wapo katika bahari ya maji chumvi.

Waliopigia kuwaoamba msaada walichofanya ni kuwaambia washushe ndoo katika maji waliyokuwa wakisafiria kuchota maji.

Hata hivyo, pamoja na habari hiyo njema iliyotangazwa na serikali , lakini wasiwasi wetu watanzania ni kuwa , serikali imekuwa na kawaida ya kupanga mipango mingi ya maana lakini utekelezaji wake umekuwa ukibaki katika makablasha wizarani.

Pia mawaziri wengi wamekuwa hodari wa kueleza mipango mingi inayotekelezwa na serikali bungeni wanapojibu maswali ya wabunge lakini mipango hiyo huwa haitekelezeki.

Naamini waziri Masha alivyoeleza nia hiyo ya serikali haikuwa akitania ni mambo ambayo yapo katika mchakato wa kukamilishwa.

Kama alivyosema kuwa serikali imeshindwa kukubali zabuni ya mwekezaji mmoja ambaye aliiwekea sharti kupewa ukiritimba kusambaza kwa watumia yeye mwenyewe.

Masha alisema wizara yake inawasiliana na wizara ya fedha kuweka vivutio kwa wawekezaji na watumiaji hasa kutokanana gharama kubwa za usambazaji wa gesi asilia.

Alisema sera nzuri na vivutio vitaiwezesha serikali kuhimiza kwa ufanisi matumizi ya gesi asilia kwenye gari na kwa ajili ya kupikia na kuokoa fedha za kigeni kuagiza mafuta na kupunguza matumizi ya kuna na mkaa.

Tuaamini kuwa umakini huo utasaidia kupatikana mzabuni bora na kwa haraka ambaye atasaidia kuwaondolea kero watanzania.

Lakini wakati tukisubiri neema hiyo, serikali pia haina budi pia kubuni nishati nyingi mbadala za mafuta kama vile kuanzisha viwanda vikubwa kwa ajili ya kusindika mbegu za mti wa Jatropher ambao unatoa mafuta ya diseli na malighafi kwa ajili ya kutengenezea sabuni.

Mti huu unastawi kila mahali hapa nchini na kwamba una sifa moja kubwa kuwa unaweza kuvumilia unaweza kustawi hata katika sehemu ambazo ni kame.

Kuanzisha viwanda hivyo kutasaidia kuongeza uzalishaji wa mafuta ya diseli hapa nchini pamoja na kuongeza ajira kwa mamilioni ya watanzania.

Nasema itaongeza ajira kwa sababu asilimia 60 ya watanzania wanaishi vijijini ambako kilimo cha zao hili ndiko kitafanyika kwa wingi.

0 Comments:

Post a Comment

<< Home