Nguvu za soda za serikali kuhusu wamachinga
KAMA kuna kitu ambacho watanzania sasa wamekingundua ni jinsi serikali yao inavyoendesha mambo yake kwa mtindo wa zima moto.
Wameshaelewa kuwa kama kuna amri itatolewa na viongozi wa juu wa serikali, basi amri huyo ni ya kupita tu, mara nyingi huwa hakuna ufuatiliaji wa karibu.
Sijui ni watendaji wa viongozi hawa ndio wanaowakwamisha ama ni viongozi wenyewe wanatoa maagizo mengi mno kiasi kwamba mengine wanajikuta hawayakumbuki tena. Ama maagizo haya yanatolewa tu kwa sababu viongozi hawa wanataka kuonyeshwa kwamba wanafanya kazi.
Kwa hakika hakuna majibu mwafaka ambayo yanaweza kupatikana kwa urahisi labda tu viongozi hawa watuambie.
Kilichgonisukuma kuandika mambo haya ni ukweli ulianza kujionyesha katika kushindwa kwa agizo la wamachinga tu la kuwaweka katika maeneo maalum waliyopangiwa jijini Dar es salaam.
Operesheni ya kusafisha jiji la Dar es Salam iliyoendeshwa Oktoba mwaka jana, ilifanikisha kuwaondoa wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kwa jina la wamachinga katika maeneo yasiyoruhusiwa kuendesha shughuli zao.
Pia waliokuwa wamejenga maduka, vibanda na aina zote za majengo kwenye maeneo ya barabara, nao walivunjiwa. Hatua hii ilipendezesha jiji la Dar es Salaam kwa kiwango cha juu kabisa ambacho kwa mingi iliyopita hali hiyo haijawahi kufikiwa.
Operesheni hii ilisimamiwa kikamilifu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro, ambaye alikuwa akitekeleza maagizo ya Rais jakaya Kikwete na kupitia kwa waziri Mkuu, Edward Lowassa.
Baada ya hatua hiyo, mgambo pamoja na askari polisi walimwagwa kila mtaaa kuhakikisha kuwa hakuna mmachinga ambaye anarejea katika maeneo hayo tena.
Mbali ya kumwagwa askari mitaani pia tulishuhudia viongozi karibu wote wa serikali wakitoa maagizo na tambo nyingi kwamba chinga hawatarejea katika maeneo hayo kamwe. Tukasikia kitu kingine kwamba ili kuwafanya wamachinga wafanyie shughuli zao katika eneo lililo bora jengo la kisasa linajengwa Karume.
Waziri mkuu Lowassa alienda mbali zaidi ya kuagiza manispaa za jiji kuanzisha bustani katika maeneo ambayo yaliyokuwa yakitumkiwa na wamachinga, lakini hata hilo halijafanyika.
Yakaisha tukasubiri kuona utekelezaji wake, lakini kama ilivyo kawaida kwa maagizo mengi ya serikali ambayo huwa hayachelewi kupuuzwa , taratibu tulianza kuona mmachinga mmoja mmoja anarejea mitaani na sasa wamejazana tena kama zamani.
Wengine hivi sasa wapo katika harakati za kuanza kujenga vibanda katika maeneo yale yale waliyondolewa, serikali ipo, haichukui hatua. hii inoanekana kama vile juhudi zilizofanyika kuhawamisha zilikuwa sawa na nguvu za soda aina ya coca cola ambayo hufoka mara ikifunguliwa baada ya muda inatulia.
Ni wazi kuwa kazi hii si nyepesi hasa kutokana na usugu uliojengwa na wamachinga kwa miaka mingi kwamba wana haki ya kuvunja sheria na hakuna watakalofanyiwa na vyombo vyenye mamlaka ya kusimamia miji yetu.
Nenda hivi sasa katika mitaa ya Kariakoo – mzunguko wa shule ya Uhuru, Kariakoo Sokoni na mtaa wa Msimbazi, Tandamti, Pemba Ubungo stendi ya daladala hapa nataja kwa uchache tu, bishara wa wamachinga inaendelea kama kawaida.
Wamachinga wanaodai kuwa maeneo waliyopangiwa hayana biashara na kwamba hata miundombinu haipo kama vile stendi ya mabasi ambayo huwa ni kigezo kikubwa cha kupata wateja. Wamachinga wanaolalamika haya ni wale ambao wapo katika soko la Kigogosambusa.
Ni wazi kuwa sulala la wamachinga sasa serikali ya awamu ya nne inapaswa kuonyeshwa kwamba, maagizo ya serikali sio ya kuchezewa ovyo voyo kwamba inapotoa maagizo yake yanapaswa kutekelezwa.
Awamu ya nne imekwisha kutagaza wazi azima yake ya kuhakikisha kuwa inatekeleza mambo yake kwa kasi na kufuata sheria na kwamba watedaji ambao watashindwa kutekeleaza maagizo ya viongozi wa juu watafukuzwa kazi.
Tunaasubiri kuona suala hili la wamachinga kujua ni nani ambaye amezembea mpaka kusababisha watu hawa wakatoka katika maeneo waliyopngiwa na kurejea mitaani kufanya shughuli zao.
Kandoro ambaye ameonyesha kuwa anauwezo wa kuongoza mkoa wa Dar es Salaam tangu aingie, tunadhani hili la wamachinga kurejea mitaani litakuwa ni mtihani wake mwingine kuonyesha kuwa anaweza kusimamia maagizo ya wakubwa wake barabara.
Kushindwa kwa suala hili ni aibu kwa rais Kakaya Kikwete na waziri mkuu wake Lowassa ambao sulala hili tangu waingie madarakani mwaka mmoja uliopita wamelivalia njunga. Pia itakuwa ni kuonyesha kuwa sasa serikali yao imekwama kutekeleza maamuzi yake yenyewe.
0 Comments:
Post a Comment
<< Home