Mzee wa tafakari

Tuesday, February 06, 2007

Kificho na mtego wa panya

WIKI hii Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho alimzuia waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi kupiti Chama cha Wananchi (CUF), Abasi Muhunzi, kutoa hotuba yake kabla ya kuiwasilisha kwake kwa madia ni utekelezaji wa kanuni za Baraza.

Kificho bila ya kuficha alisema agizo lake la kutaka kuziona bajeti za wapinzani kabla hazijawasilishwa barazani litaendelea kuwako na kamwe Baraza lake halitastahimili kauli za matuzi na kejeli. 
Alisema kumekuwako na vitendo visivyovumilika vinavyofanywa na mawaziri kivuli vikiwamo kutoa lugha za kebehi zinazokwenda kinyume cha kanuni.

Alinukuu kanuni ya 151 inayosema kama kutatokea mambo ambayo kanuni yetu haikusema, basi Spika ndio mlezi mkuu wa kanuni zetu, ingawa kanuni hizi ni mali ya wajumbe wote,” alisema Spika Kificho.
Kwa hakika kitendoi hicho kimenikumbusha hadithi ya mfalme na mtego wa panya.
Msomaji wangu sio vibaya nikieleza kwa kifupi hadithi hii ambayo inafanana sana na mamabo ambayo yanafanyika zanzibar kwa sasa.

Mfalme Siku nyingi alikuwa mkulima mzuri wa mahindi na mazo mengine ya nafaka.
Kila mwaka alivuna mazo mengi na kuyahifadhi katika ghala kubwa nyumbani kwake. Kutokana na ukulima huoalisifika sana katika katika eneo lake.

Hata hivyo, alikuwa na amatataizo kadha aambayo yalikuwa yanamsumbua. Mojawapo lilikuwa ni panya wengi waliokuwa wakila nafaka zake ghalani.

Baadaye panya kumsumbua kwa muda mrefu aliamua kutafuta mtego wa kuwanasa. Mtego huo aliuweka mahali ambako palikuwa ndio njia ya panya kuingia ghalani.

Panya kama kawaida yao walipoamua kwenda kula nafalaka ghalani walikuta mtego ambao walishitukia na kuamua kwenda kutafuta chakula sehemu nyingine.

Hata hivyo pamoja na kuamua kwenda kutafuta chakula sehemu nyingine waliamua kuwaambia wanyama wengine waliokuwa wakifungwa na mfalme kama vile bata , paka, mbuzi na farasi kuwa wautegeua mtego huo kwa vile unaweza kuwanasa.
Mtengo huo baada ya siku tatu ulimnasa nyoka. Mfalme aliposikia kuwa mtego umenasa akaajua mbaya wake panya atakuwa amesaswa alifurahi na kwenda kumwangalia.

Alipofika karibu na mtego huo aliumwa na nyoka huyo ambaye baadaye aliumwa na kufariki dunia.
Baada ya kufariki mbuzi na bata walichinjwa kuwapatia chakula watu waliofika msibani na farasi akabaki mbeba mzigo huku panya akibaki hana chakula kutokana na familia hiyo kusambaratika baada ya kifo cha mfalme.

Baada ya tukio hilo, panya akawacheka wabnyama wenzake kuwa kama wangemsikiliza na kuutegua mtego huo hawangepata shida na wengine kuchijwa.

Hadithi hii inafanana sana vitendo vya ubaguzi na uchohezi ambavyo vianza kufanywa ambayo kama havitazuiwa ni wazi mambo makubwa yanaweza kutokea
Kitendo cha Spika Kificho kudai hotuba za wapinzani azipitie kwanza ni mwanzo wa chokochoko wa hali iliayoanza kutulia visiwani.

Sioni sababu iliyomfanya Kificho kuamua kudai kwanza kuziona hotuba zao wakati hakuna kigezo kama hicho wakati wanapochangia hoja zao bungeni.

Mbunge ni mtu mzima ambaye anajua wajibu wake hawezi kuzungumza maneno ya kejeli na au kutukana wakati akijua wazi kuwa kuna kanuni ambazo zinambana kufanya hivyo.

Kificho anapaswa kusimamia kanuni zote za Baraza hilo na kuwaacha wapinzani wawe huru kutoa mawazo yao ya upinzani bila ya kuwasilishwa kwake kwanza.

Msimamo huo wa Spika unaonekana wazi kuwa sasa jahazi la zanzibar ambalo lilikuwa liyumba kwa muda mrefu lianza kukaa sawa majini analitoboa ili lizame.

Kwa hakika kama chokochoko zinazofanywa na kificho dhidi ya wawakilishi wa CUF kama hazitazuiwa mapema basi, matatizo makubwa yatatokea.

0 Comments:

Post a Comment

<< Home